Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umetangaza majina ya waliofuzu kwenye shindano la kitamaduni, kuhusu kumbukizi ya kuzaliwa Mtume Muhammad na mjukuu wake Imamu Jafari Swadiq (a.s).
Shariti la kupokea zawadi, mshindi anatakiwa afike yeye kupokea zawadi katika hafla itakayofanywa mbele ya mlango wa qibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) siku ya Jumapili 16/Rabiul-Awwal/ 1448h, sawa na 30/ 08/ 2026 saa 2:30 jioni.
Iwapo mshindi atapata udhuru na kushindwa kufika kwenye hafla, atatakiwa aende katika kitengo cha wahasibu wa Atabatu Abbasiyya ndani ya muda usiozidi wiki mbili kuanzia tarehe ya kutangazwa matokeo, akiwa na nyaraka zinazomthibitisha (kitambulisho cha taifa au hati ya kusafiria).
